Saturday, June 12, 2010

Monday, March 29, 2010

NYERERE KUPANDA LIGI KUU MSIMU UJAO

Timu ya soka ya nyerere ya mkoani kilimanjaro iko katika mikakati kabambe ya kuhakikisha inarejea kwa kishindo katika ligi daraja la kwanza, inayotarajia kuanza september mwaka huu.



Meneja mipango wa timu hiyo, yenye maskani yake, kata ya kaloleni mjini Moshi, Yusuph Masanja amesema kwa sasa viongozi wako katika mikakati kabambe ya kuhakikisha kuwa azma ya kupanda daraja kucheza ligi kuu inafikiwa.



Masanja amesema kupitia vikao vya kamati ya utendaji, wameteuliwa watu watano kukutana na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Monica Mbegawa, kupanga mikakati ya kutafuta vyanzo vya fedha vitakavyoisaidia timu hiyo.



Timu hiyo ilifanikiwa kubaki ligi daraja la kwanza msimu uliopita, baada ya kushika nafasi ya saba kati ya nane, na kuicacha segera ya tanga ikishuka daraja.



"hatukufanya vizuri msimu uliopita kwa sababu ya ukata na kukimbiwa na wachezaji wetu, lakini sasa tumeamua kufanya maandalizi ya mapema ili kuhakikisha hatupati matatizo kama yaliyotukuta mwaka jana"alisema masanja.